1 Wakorintho 1:4

"Namshukuru Mungu siku zote kwa ajili yenu, kwa sababu ya neema ya Mungu mliyopewa katika Kristo Yesu"

MOYO WA IBADA 2024

Bwana Yesu Asifiwe Sana!

Kipekee tunamshukuru Mungu kwa kutupa kibali na NEEMA ya kumfanyia Ibada kubwa ya SHUKRANI. Ibada ya Mwaka huu ni ya Kumpelekea Mungu Shukrani tukiongozwa na Neno la Mungu kutoka 1 Wakorintho 1:4 "Namshukuru Mungu siku zote kwa ajili yenu, kwa sababu ya neema ya Mungu mliyopewa katika Kristo Yesu"

Kamati ya maandalizi inapenda kukualika kuungana nasi katika kufanikisha jambo hili lenye baraka la kumuandalia Mungu Ibada. Ibada hii inatarajiwa kufanyikia uwanja wa tanganyika Peckers, kawe Dar es Salaam mwishoni mwa mwaka huu 2024.

Tunatanguliza shukrani zetu za dhati na Mungu akubariki sana.

FOMU YA SADAKA YA IBADA

Endapo utapenda kutoa sadaka yako kwa ajili ya ibada hii, tafadhali jaza fomu hii chini kisha fuata maelekezo ya namna ya kutuma sadaka yako.